LEO TAREHE 20 OCTOBA NI SIKU YA KIFAHARI KATIKA HISTORIA YA NCHI YA KENYA

Ni wazi kuwa tangu nchi ya Kenya kupata Uhuru kutoka kwa mabeberu leo hii ni siku muhimu kwani waliopigania ukombozi wa nchi wanakumbukwa na kufanyiwa heshima kubwa kisherehe.

Akiongoza sherehe hizo uwanjani NYAYO, Rais Uhuru Kenyatta, amezungumzia mambo muhimu ya kukuza umoja wa nchi. Rais Kenyatta amegusia masuala ya Uchumi, Siasa, Afya na Utangamano. Amezungumzia mambo yanayokwaza ukuaji na maendeleo ya nchi miongoni ikiwa ni Tatizo la Ugaidi, ulevi, na uwindaji wa wanyama pori.

“NI matumaini yetu sote kusitisha changamoto zinazokwamisha azimio na malengo yetu!”

Embedded image permalink

“Lazima tupinge mambo yanayoleta utengano na uasi nchini Kenya: Lazima tukuze mambo yanayoleta umoja na upendo miongoni mwa kila mwananchi” alisema Kenyatta.

Siku hii ni muhimu sana kwani inaleta picha ya Uhuru wa nchi  na mabadiliko tokea upatikana kwa katiba mpya kwa sababu inahadhimisha miaka 52 ya uhuru.

Sakata nzima NYS yaani Huduma kwa vijana imeangaziwa kwa kina na suala ya elimu kwa kuwa ni msingi wa maisha ya kila mtu. Miongoni mwa vikwazo vya maendeleo kataja mizozo ya mipaka, ukabila na ufisadi.

“Ni muhimu kufanya kazi kwa pamoja na kushirikiana “Uhuru kazungumza kwenye hotuba yake.” Msijali kuhusu mambo ya ICC, kwani tutazidi kuomba “akaongezea Rais.

mashujaa waliotangulia, waliopo kwa sasa wanazidi kusherekiwa kwenye uwanja wa ICC. Wanamichezo, wanasiasa, wanahabari, na pia vijana mahiri wanozidi kujituma wana siku kuu leo.