Serikali imetangaza kufanya siku ya Alhamisi 26, kuwa siku kuu na siku ya maombi nchini huku mtakatifu Papa Fancis akiwasili nchini kenya.

“kama tumebahatika kutemelewa na mtakatifu Papa, ataongoza shughuli za siku hio” msemaji wa Ikulu ya Rais Manoah Esipisu alisema wakati akisambaza habari hio kwenye vituo vya habari.

Papa anatarajiwa kuwasili Nairobi Jumatano jioni kwenye ziara yake ya siku tatu na awamu yake ya kwanza barani Afrika.

Atatua katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) mwendo wa saa kumi na moja jioni (5pm).

Ziara yake nchini itakuwa moja wapo wa atua muhimu. Papa John II alizuru Kenya miaka ya 1980,1985 na 1995.

Atakapokuwa nchini, Papa atashirikiana na wakenya kwenye Misa, kufanya vikao mbalimbali na Rais Uhuru Kenyatta lakini pia na viongozi wa dini, vijana, na pia kujumuika na watu wa kawaida kimaisha yaani makabwela wa jamii.

Baada yaKenya Papa anatarajiwa kusafiri Uganda na kukamilisha ziara yake kwenye nchi Jamhuri ya Afrika ya Kati.

1 COMMENT