Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Hamonize akiwa na mtayarishaji wa wimbo Aiyola,

Msanii anayetamba kwa wimbo wa “Ayola” nchini Tanzania chini ya lebo ya Wasafi Classic, ameibuka na jipya tena kwa kudai kufanya kazi na watayarishaji wadogo kwenye industry.

Harmonize amesema kufanya kazi na watayarishaji wakubwa wenye majina tajina itamchukua muda kwani anahofia kutomtendea producer kubwa haki kwani ni gumu kushaurina nao ilhali wale wachanga wanaweza kushauriana maambo mengi tu.

Aliyazungumza  hayo kwenye kipindi kimoja cha Clouds FM wakati akiutambulisha wimbo wake mpya ‘Bado” aliomshirikisha boss wake Diamond Platnumz.

Wimbo mpya wake Harmonize umetayarishwa ndani ya wasafi studio chini ya Producer Lizer Classic huku ngoma yake Ayola iliyomtambulisha iliandaliwa kwenye studio ya Kazi Kwanza Records chini ya producer Maxmaizer.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.