Mkali wa ngoma,’Utanipenda’ ameamua kufanya kile ambacho wengi wa wasanii maarufu ukifanya kwa kisingizio cha ustaa.

DIamond Platnumz ametoboa pua yake na kuweka kipini kitu ambacho wengi wa mashabiki na mahasimu wake wanakichukulia poa tu.

Diamond_Platnumz_Nose

Kwa sasa wengi wanajiuliza maswali mengi kuhusu uamuzi wake wa kutia vipini puani. Baada ya kupiga picha hio, alirudi tena na kutupia mtandaoni picha bila hicho Kipini.

Diamond_Platnumz_Face

Hata hivyo kwake sio tatizo kwani hata mastaa mbalimbali huwa nazo kama,Chris Brown,2Pac,Davido na wengine wengi.

Baada ya tukio hilo la jana, ilizuka tafrani nyingi kwenye mitandao huku wengi wa mashabiki na washikaji wake wakikashifu hatua hiyo aliochukua kwani ni kinyume na sheria za dini ya Kislamu.

Diamond_Platnumz