Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Msanii anayetamba sana kwa muziki wa Bongo Flava Afrika na duniani alitangaza utajiri wake majuzi kuwa ana takriban $4Million na kuwaacha watu na dukuduku.

Diamond Platnumz amekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari kuhusiana na utajiri wake huo lakini pia picha ya vuvu la kichwa cha mtu ambalo lilionekana mezani wakati alikuwa anatia sahihi yake kwenye mkataba na Ketchup watengenezaji wa bidhaa nchi Tanzania na akaamua kuanika picha hizo kwenye mitandao ya kijamii.

Diamond_Platnumz_Deal

Diamond anahusishwa sana na Uchawi na Wanga huku mashabiki na mahasidi wake wakidai ni kama ni mwanachama wa kundi la Illuminati ili kujipa sifa na kutajirika kiasi hicho.

Shutma hizo zimemfanya mkali huyu wa ‘Utanipenda’ kujibu na kukanusha madai hayo huku akisema hilo ni pambo kama pambo lingine tu.

“Ni urembo au pambo kama mapambo mengine, hakuna kitu kama hicho.
Usidanganyike, hakuna anayeweza kumuweka mtu juu zaidi ya Mwenyezi Mungu.

Mimi naswali sana na namtegemea Mungu kwa kila kitu na kweli ananipigania.
Unajua watu wengi wamekuwa wakizungumza oooh…natumia uchawi lakini ukweli ni kwamba maombi, ubunifu, juhudi na heshima ndivyo vitu vinavyoweza kumfanya mtu yeyote kupata mafanikio katika kitu akifanyacho au jambo alifanyalo.”

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.