Msanii wa kike wa Bongo Fleva ambaye anafanya vyema kwenye tasnia ya muziki amekerwa na hatua ya Kundi la muziki la ‘Yamoto’ kushoot video yao ya pamoja bila uwepo wake.

13408772_1025492654193103_826974025_n

Ruby ambaye ameshirikishwa na Yomoto Bend alisimulia  hali aliyokuwa nayo huku meneja wa Yamoto Bend Said Fella akisema kuwa siku ya kufanya video hio kwa jina ‘SU’  Ruby alikuwa na “Stress” kitu kilichomfanya ashindwe kutoke kwenye maeneo ya tukio.

Msanii huyu amefunguka yote hayo wakati wa mahojiano kwenye kipindi kimoja cha radio nchi Tanzania kuwa wakati wa kufanya video hio yeye alikuwa na majukumu mengi ila akawaomba kama Yamoto wangemsubiria kama alivyowasubiria wao wakati wa kurekod Audio hio japo kuwa hawakufanya subira wakaishia kushoot Video

“Nimeumia sana maana audio ile tumefanya muda mrefu na waliweza kusubiri mpaka tukakamilisha iweje kwenye video washindwe kunisubiri, maana hii kazi tunasaidiana,” alisema Ruby.

Hatua hio kwake Ruby haikuwa sawa kwani hawakuafikiana kushoot bila yeye kwani kwenye nafasi yake ameoneka mrembo mwengine akiimba sehemu yake.