Kila kukicha kuna wasanii wapya kwenye soko la muziki wanaochipukia na kuja kwa kasi mno. Wasanii wa Nyimbo za ‘Gospel’ wanajitahidi kinoma kuteka anga za burudani kwa kazi zao matata za kuvutia kila mtu.

Beryl Nabby ni chipukizi kwenye hii tasnia ya muziki anayefanya vizuri na nyimbo tatu za aina ya Gospel kwa sasa-Nikupe Nini, Jesus I Love You na Praise You.

Ni mzawa  na mkulia dini kutoka Kaunti ya Busia kwenye familia ya watoto wanne;madada watau, mvulana mmoja. Mwimbaji huyu jina lake halisi ni Beryl Birenge aliyeupenda muziki tangu utotoni mpaka shuleni na kanisani alikuwa mwana kwaya.

Beryl aliingia studioni kurekodi wimbo wake wa kwanza ‘Nikupe Nini’ miaka minne iliopita ndani ya Tracklab Studios.

Kwenye mahojiano katika kipindi cha Ukumbi Wa Vijana Jumamosi tarehe 18/7/2016 kupitia Ecn Radio 99.9fm, alisimulia jinsi alivyotoka kimuziki na baada ya hapo alijipa pumziko kwa miaka minne wakati alipokuwa ‘college’ kisha akarudi kufanya video ya wimbo ‘Jesus I love You’ aliyomshirikisha msanii Real G huku mwongozaji wa video akiwa ni Daudi lakini pia kurekodi nyimbo nyingine ‘praise you’.

“Be faithful to God always, he hears you, He will answer in the right time”. alisema Beryl

Beryl ni msanii mahiri mwenye uraibu wa Reading, Swimming, Singing,Watching Movies na pia Dancing. Na kwa kuwa ni msanii ambaye ni mcha mungu na pia mfuasi wa dini,ni mwenye kujituma kwani ana malengo ya kufungua kituo cha kuwashughulikia na kuwajali watoto mayatima na wale wa mitaani ‘Childrens Home’ siku za usoni.

Video ya ‘Praise You’ nayo imeachiwa tayari huku Audio na Video yake ikiongozwa na Track Lab.