Muziki ni ni kipaji lakini pia ni ajira kwa watu wengi wanaoutegemea kwa ajili ya riziki na kujikimu maishani.


Kwa kawaida wasanii wengi duniani ni wa kiume huku wachache wakike wakiwa wanajitahidi kupenya kwenye ulingo huo wa burudani. Mwimbaji mwenye kipaji na ambaye pia ni mwana mitindo yaani Fashion Model amekuwa akipambana kwa kila mbinu kufikia hatua aliyo nayo kwenye mafanikio yake maishani.

Wayinke-Fashion Model

Wayinke ni Fashion Model ambaye ni mlimbwende mwenye sura ya malaika tena mwimbaji aliyeanza muziki kwenye umri mchanga. Amekulia kwenye dini kwani mamake mzazi ni Kasisi wa kanisani mazingira yaliyomsaidia kutunga nyimbo zake.

Tangu alipokuwa shule ya msingi darasa  la saba hadi kidato cha nne alikuwa akihimizwa na waalimu kujiunga na Drama Clubs, School Choir, na hata Music Clubs kwani sauti yake ilitosha kumtoa nyoka pangoni.

(Wayinke kwenye Ubora wake)

Wayinke amekuwa kwenye kundi la muziki kwa jina la Afrizo la mmoja wa wahadhiri wa chuo cha Nairobi ,Hellen Mtawali alikosomea digrii ya masomo ya biashara ila kwa sasa yupo tayari kurekod nyimbo zake pekee na pia anaomba support yoyote ile.

“Nilianzisha Wayinke Youth Foundation kwa  lengo la kusaidia vijana kwenye jamii kupitia kwa program maalum kama vile, Health, Education, Arts an Culture ili kusaidia vijana wengi wenye talanta mbalimbali.” Wayinke alisema.

Kwa upande mwingine, Wayinke ametia fora kwenye Modelling huku akiibuka kwenye nafasi ya 1st Runner Up Miss  Tourism Nairobi Kenya mwaka 2013/2014

Mwaka 2014,kwenye Goodwill Modelling kitengo cha Miss Cultural Heritage Nairobi alishinda tuzo hio kama balozi wa Utamaduni na Turathi huku pia akipata shavu kwenye matangazo ya Coke Studio Afrika kama Singing Model

Aliachia kibao chake cha kwanza,’Ni Yeye’ kilichotayarishwa na RKelly na video yake kuongozwa na Johnson Kyalo.

Tazama Video yake hapa chini:

Miss Heritage and Cultural Ambassador huyu amehusika kwenye kampeni nyingi za mashuleni ili kupiga vita matumizi ya mihadarati na ulevi miongoni mwa wanafunzi.

1 COMMENT