Tecno Camon C5 ni bonge moja la simu ya aina ya Smart Phone ambayo ina tamba sokoni kwa sasa kwani features zake ni za kisasa na za kuvutia.

Tecno Camon C5 2

Kampuni ya Tecno ambayo ni mabingwa wa kutengeneza simu nzuri, imekuletea simu hii yenye ubora wa kupiga picha kwani Camera yake ni pixel 720 x 1280 resolution na screen ya 5 inch.

Tecno Camon C5 1
Tecno Camon C5 yenye 5 Inch

Camon kama jina lake ina maana ya ‘Camera’ ‘On’ huku camera ya mbele ikiwa na 2MP na ya nyuma 8MP. Ni simu yenye uwezo na ya kwanza kwa kampuni ya Tecno kuweza kuunganishwa na mtandao wa nguvu na kasi zaidi wa 4G LTE.

Battery yake ipo imara yenye nguvu ya 2500mAh yenye uwezo wa kumudu kasi ya mtandao wa 4G . Lakini pia ina Quad- Core processor ya 1.3GHz na 8GB nafasi ya ndani ya kuhifadhia ‘data’ na pia Slot nyinge ya kuongezea Memory Card na RAM ya 1GB.

Tecno Camon C5 ina aina mbalimbali za rangi kama vile,‘Midnight Black, Dark Blue, Amber Gold, and Oyster White’.