Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Kundi la muziki maarufu kwa jina la Elani waliungana mwaka 2008 katika Alliance Française jijini Nairobi. Mwanzo wao walikuwa watu watano kwenye Bendi yaani Wambui Ngugi, Maureen Kunga, Brian Chweya and Daniel Kimani . Mwimbaji Kimani alitoweka na mpaka sasa hajulikami aliko. Elani walionyesha uwezo wao mwaka 2010/2011 wakati walipo amua kuupaisha Muziki wao kwenye hatua nyingine.

Mnamo mwaka 2013Bendi hii iliachia kibao chao cha kwanza  “Jana Usiku”. March  2014, Elani waliachia ngoma yao ya pili kwa jina  “Milele  wimbo unaozungumzia wapenzi wawili wanaoishi kwa kutojitambua huku familia ya mwana dada huyo ikijaribu kumunganisha na Daktari ili awe mpenzi wake. Video hio ilitengenezwa na mmoja wa wana Sauti Sol, Savara Mudigi akishirikiana na Sol Music Entertainment and na kuongozwa  Enos Olik . Katikati ya mwaka 2014,watatu hao waliachia wimbo wa “Kookoo”,na kufanyiwa Video kwenye mitaa ya Nairobi,wimbo ulioleta mafanikio si haba kwenye Bendi hio kwa sababu ilikuwa wimbo uliopendwa kuskizwa na kupakuliwa kwenye mitandao mbalimbali. Hatua hii ilifanya ngoma “Kookoo”kuorodheshwa nafasi ya pili kwenye Chart baada ya wimbo wa Bahati-Barua .

Bendi hii ya Elani pia ilioachia nyimbo zifuatazo “hatua”, “Zuzu “Uko Wapi”, “Barua ya Dunia” na “Mahindi. Mwaka 2016 Elani walimshirikisha  msanii kutoka Uganda Jose Chameleone kwa wimbo “My Darling”

​Kwa upende mwengine kulizuka Tafrani mwaka  January 12,2016, wakati Elani wauweka ujumbemtanadao wao wa  YouTube na mitandao yao ya kijamii wakiwashtumu chama cha kulinda haki za kimuziki za wasanii nchini MCSK kwa kutokuwa waaminifu kwani waliwalipa takriban 31,000 kama mazao ya kazi zao kwa kuchezwa kwenye Televisheni na Radio. Baada ya kuwasilisha malalamiko yao kwenye MCSK, Brian mmoja wa Elani aliitwa na Viongozi wa MCSK na kuongezewa  KES 300K, kitu kilichozua hali ya kutoeleweka kuhusu malipo hayo ya pembeni. Hata hivyo Chama Hicho kilijitetea kwa kudai kuwa Elani walitia chumvi lakini pia kuungama kuwa wao waliwalipa Rubuni ya ngoma zao baada ya kugundua kuwa hawakujumuisha malipo ya Elani ya mwaka  July 2013 hadi  June 2014 kwani nyimbo zao zilichezwa sana kwenye vyombo vya Habari na kusema kuwa kosa kama hilo halijatokea kwa Elani pekee lakini pia kwa wana muziki wengineo.

Kwa sasa wana Wimbo Mpya unitwa ‘ Sirudi‘ wameshirikisha msanii Wa Kenya Jaguar

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.