Hey! Jamani machizi mashabiki na wadau wa muziki sijui Kama huwa mnaona au kuhisi kuzinguliwa na hawa wasanii wetu wanapopanda Stage kutoa burudani?

Live kwa Stage

 

Washikaji zetu hawa wanapanga Shows ili sisi mafans tupate raha wakati wakiwa wana perform live na pia huwa tunalipia kiingilio.  Muda wote stegini huwa wanatushurutisha na kutushinikiza kuimba nyimbo zao hata Kama msanii ni mgeni au hatujui nyimbo zake.

Utaskia maneno Kama‘ Tuimbe wote’ Hapo Vipi’ ‘ Au Sio’ ‘ Yo! Yo! huku washabiki wakiwa wamelipia show hio ili kumwona Msanii akiimba mwenyewe mwisho wa siku wanaishia kuimba mafans.

Kitu cha ajabu na kustaajabisha ni pale Msanii ana Fanya show kwa dakika 10 tu na kuondoka majukwaani na kuaacha mashabiki wakikodoleana macho na kuimba wenyewe kwa wenyewe kwani ilishakuwa hali ya kawaida kwenye show za kisasa.

Je, hio ni sahihi kwa muziki wetu na mashabiki wenye mioyo wa kuonesha Upendo muziki na kuupa shavu?

Ewe nawe shabiki unaruhusiwa ubwage comments zako hapa ili tunyooshe mambo haya na kukuza Sanaa yetu.