Nyota Ndogo anafahamika kwa jina halisi kama  Mwanaisha Abdalla, aliyezaliwa mwaka 1981.Ni msanii wa  nchi kenya anayefanya aina ya muziki wa Pop Music unaochanganywa na Taarab

Nyota Ndogo

Nyota Ndogo anatokea sehemu za Pwani  kaunti ya Mombasa. Aliachia masomo ili kujitafutia maisha  huku akifanya ujakazi . Babake Nyota Ndogo mzee Abdala Atib naye alikuwa msanii kipindi cha nyuma  na hata aliongoza Bendi ya muziki ila hali hio haikumfanya Nyota Nogo kupata hamasa ya kuingia kwenye tasnia ya muziki hadi pale aliposkia na kuguswa na nyimbo za kundi la muziki wa Hip Hop la K-South wakati Producer wa Muziki Andrew Burchell akigundua kipaji chake cha kuimba.

ttt

Nyota Ndogo

Nyota Ndogo kwa sasa ameacha takribani Albam 4, kama:” Chereko, Nimetoka Mbali Mpenzi na Mama Wakambo”, Aliwahi jishindia tuzo ya Kisima Awards akiibuka kama msanii bora wa Taarab mwaka 2003 na pia msanii bora wa kike 2005. Baada ya hapo aliteuliwa katika nafasi 3 tofauti kwenye tuzo za Kisima Awards.mwaka 2008 Ikumbukwe aliwahi pia kuteuliwa kuwania tuzo za msanii bora wa kike nchini Kenya  PAM Awards mwaka 2007. Hata hivyo wimbo wake wa Watu na Viatu  ulichaguliwa bora kwenye kitenge cha Wimbo Bora wa Afrika Mashariki mwaka 2007 kataka Tuzo Tanzania Music Awards

Isitoshe, Wimbo wake wa “Take Care“umeshirikishwa kwenye album za Kimataifa Duniani mwaka  2003 huku “Chereko” ikitamba kwenye chati za muziki za Kenya.

Hijatosha aisee amemshirikisha Nonini kwenye wimbo wake “Nibebe” lakini pia Necessary Noize kwenye Track yake ya “Nataka Toa. Nyota Ndogo aliwahi mshirikisha mwana muziki Ally B kwenye ngoma iliotesa kwenye kanda ya Afrika Mashariki. Kwenye collabo nyingine na msanii Q Chilla kutoka Tanzania ilikuwa bonge la ngoma kwani ilimpa shavu kufanya kazi na Mr. Blue na ambaye ni mwamba kwenye muziki wa Bongo Fleva. Na kwenye kazi zote hizo za uhakika aliweza kupata Zali kuteuliwa kutumbuiza kwenye tuzo za Kilimanjaro Awards. Mwaka wa  2013 Nyota Ndogo aliwashirikisha Tember ambaye ni msanii kutoka bongo lakini pia msanii  Bobby Mapesa wa Kenya kwenye ngoma yake “Nawachanganya.”

ghjm
Nyota Ndogo

Nyota amewakilisha nchi ya Kenya kwenye matamasha tofauti Afrika Mashariki kama vile   Sauti za busara na  Ziff huko  Zanzibar. Amepeperusha bendera ya nchi yetu pande za Comoros. Nyota amejituma mpaka kupata shows Dubai, Germany, na  South Africa. Kama ulikuwa ufahamu basi mkali huyu aliwahi kuwa mtangazaji kwenye kituo cha radio cha Baraka Fm huko pande za Mombasa Kenya. Mwaka  2013 alikuwa miongoni mwa majaji wenye mojawapo ya Show kubwa kwenye Tv katika Afrika Mshariki za “Tusker Project Fame”.Kwenye mwaka wa 2013  pia alishinda tuzo za msanii bora wa kike kutokea  Pwani

nyota ndogo

Nyota Ndogo