Avril ambaye ni mwimbaji wa ngoma ya ‘No Stress’ aliyomshirikisha msanii wa Tanzania AY huenda akawa amepania ujio mpya na msanii wa Hip Hop Darassa  kutoka Tanzania tena.

Darassa na Avril

Avril alitua nchini Tz kimya kimya kwa ziara zake za binafsi lakini amekuwa akionekana na baadhi ya wasanii wakubwa huko kitu kinachotabiriwa kuwa kuna collabo itafanyika na mkali  huyo wa ‘Kama Utanipenda’ akishirikiana na Rich Mavoko ‘ Too Much’ anayefahamika kama Darassa

Wawili hao wameonekana pamoja kwenye studio Moja na producer Abbah .Avril ni msanii wa kike nchini Kenya anayefanya vizuri kwenye Tasnia ya muziki nchini na pia majukwaani anakopenda kuonyesha maungo yake ya mwili kwa kuvalia mavazi ya kumtia aibu mbele za mashabiki na washika dau wa muziki.

Avril