Msanii na Rais wa Wcb Wasafi amefunguka na kuweka wazi kuhusu ujio wa mtoto pili.
Diamond Platnumz ambaye ni baba Tiffah amesema yeye na mzazi mwenzake Zari watakuwa wakitarajia mtoto wa kiume mwezi Disemba mwaka huu.

Diamond & Zari

Mkali huyo wa ‘Kidogo’ amesema baada ya Zari kujifungua kijacho watakuwa wanafunga ‘ Chapter’ ya kuzaa kwani watakuwa wametosheka na watoto wawili. Kwa mujibu wa Diamond watapata muda wa kupisha burudani kwenye familia yao huku wakila bata zaidi.

Tiffah na Diamond

Tiffah ambaye ni mtoto wa kike wa kwanza wa ‘Simba‘ anatarajia kutimiza umri wa mwaka mmoja.