Msanii wa muziki wa Gospel anilizimia kwa nyumba yake Kasarani Jumanne ya tarehe 2 katika hali ya kutatanisha.

Willy Paul aka Willy Pozee inasemekana alijikuta katika hospitali ya Mater Hospital Nairobi akipokea matibabu baada ya majirani wake kumsaidia kumfikisha humo.

Willy Paul/ Hisani ya edaily.co.ke

Mkali huyo wa ngoma ‘Fanya‘ amesema hajawahi kuzimia wala sio mgonjwa wa Pumu ila alishangazwa na hali hio kumtokea kwa mara ya kwanza.
Kwa mujibu wa daktari wake amesema kuwa kutoka na Willy kusafiri mataifa mbalimbali utofauti wa hali ya hewa na mazingira ndio sababu kuu ya hali kuzirai ghafla.

Willy Pozee ambaye ameondoka hospitalini Jumatano iliyopita anatakiwa kupumzika kwa nyumba kuuguza majeraha aliyopata kwenye mkasa huo. Japo kuwa mkali huyo ndiye msakatonge kwa nyumba yao anatarajia kuwa sawa ili aendeleze kazi zake kwani atakuwa tayari kupanda majukwaani kuanzia Wikiendi hii.

“If I made it through the tough night, then God is really good! Thank you Lord! Thank you again,” Willy Paul aliandika.

Willy Pozee

Hii ni baada ya mkali huyo wa ‘Sijafika’ kufahamisha mashabiki wake kupitia mitandao ya jamii.

Nao mashabiki hawakusita kuonyesha upendo wao kwa kumtakia nafuu ya upesi.

“GET WELL & QUICK RECOVERY”, Willy Paul.