Leo ni siku muhimu kwa familia ya Simba na ya furaha kwa binti yao kutimiza umri wa mwaka mmoja.

Latiffah Dangote Birthday

Princess Tiffah Dangote anasherekea siku yake ya kuzaliwa Leo hii kwani alizaliwa siku kama ya leo tarehe 6, Jumamosi mwezi wa Agosti mwaka Jana.
Diamond na Baby Tiffah

Diamond Platnumz hakuchelewa kuonesha bashasha yake kwa malkia huyo wake kwa kumtakia kheri njema pamoja na mzazi mwenzake Zari Hassan.
Zari na Baby Tiffah

Kupitia ukrasa wake wa Facebook Diamond aliandika ujumbe kwa ajili ya bintiye Tiffah.
Nao mashabiki na washikaji zake walipata muda wao maalum kumtakia Tiffah siku njema ya kuzaliwa na maisha marefu ya fanaka.

Mkazivae Unit nayo yamtakiwa Princess Tiffah Dangote kila ya kheri na maisha mema ya baraka.

Mkazivaeunit