Game la muziki linashuhudia mabadiliko makubwa kutokana na mwamko mpya wa wasanii kujituma kazini na kufanya kazi zenye ubora mno.

Wasanii wengi wamefanya vizuri sana kwenye tasnia ya muziki na wengine kujiongeza zaidi kibiashara, uwekezaji na pia wengine ni watetezi wa haki za muziki na wasanii bungeni.

Nchini Kenya msanii Jaguar au Charles Jagua Kanyi kwa sasa ni mbunge mtarajiwa baada ya kuteuliwa kwenye kura za uteuzi na anasubiria hatima yake Agosti 8, 2017 wakati akiwania nafasi hio ya MP wa Starehe dhidi ya wagombezi wengine.

jaguar kenya
Jaguar

Tanzania kuna wabunge wawili ambao ni wasanii nguli kutokana na muziki wao. Msanii wa hip hop bongo maarufu kama Profesa Jay au Joseph Haule ni mbunge a eneo bunge la Mikumi Tanzania. Mbunge mwingine ni Joseph Mbilinyi aka Mr. Sugu ambaye pia ni msanii wa kizazi kipya anayewakilisha wasanii bungeni.Ni mbunge wa Mbeya.

prof jay.png
Profesa Jay
sugu
Mr Sugu

Afika Mashariki yazidi kupiga hatua kimuziki baada ya kuona hamasa kutoka kwa wadau wengi wanaopigania kufikisha muziki wetu mbali. Uganga msanii Robert Kyagulanyi Ssentamu aka Bobi Wine kwa sasa amewahi nafasi ya ubunge baada ya kushinda kura kwenye uchaguzi. Anawakilisha eneo bunge la Kyandondo East Uganda.

Bobi-Wine-Sema
Bobi Wine

Tukitakie kila la kheri msanii Jaguar kwenye uchaguzi mwaka huu.

#MitegoEA.

Click: www.facebook.com/MkazivaeUNIT