Baada ya Diamond Platnumz kufungua music lebo yake ya Wcb Wasafi na pia mtandao wa kuuza muziki ili kusambaza kazi za wasanii Afrika Mashariki kwenye soko kubwa la dunia, sasa King maker Visita ana yake.

Dr. Visita aka King Maker ambaye ndiye super rapper na supper singer, amefunguka mengi ndani ya Konnect show ya Clemmo254 kupitia Radio Maisha.

Msanii huyo ambaye baada ya kuondoka GrandPa records, amekuwa kimya kimuziki licha ya kuwa yeye alifungua studio yake ‘Hela Records’ pamoja na mkali Kenrazy pamoja na mpeniz wake msanii Sosuun.

Mkazivae na Visita.

Studioni leo amekuwa na msanii wa kike ambaye yupo chini ya lebo yake hio ya Hela, anaitwa Scar ambaye walikutana wakati akitafuta msanii wa kuweka vocals kwenye project yake ya ‘Kombora‘ na hapo akafumbua kipaji chake pamoja na kuwa Scar alikuwa ana ndoto ya kuja kuwa msanii mbeleni.

Visita amesema kuwa pia yeye kama msanii yupo chini ya record lebo nyingine pamoja na studio yake, chini ya Big Dreams Entertainment alipo msanii Kush Tracey.

Clemmo 254 amehoji kuwa bado wapo na ukaribu na msanii KenRazy na kma vipi mbona hawajaachia collabo pamoja kama ilivyo desturi? “Mimi na Kenrazy tuko poa hatujakosana but kila mmoja anakaza pande yake wajua muziki ulivyo mpaka kukazana but now am concentrating on my single projects.” yeye kafunguka.

Akiwa amekuja kuzindua kazi mpya collabo na mwanamuziki huyo Scar,kwa jina ‘Utamu’ amekiri wazi kuwa yeye ni msanii wa kuimba sio kurap kama navyokuwa akifanya tangu atoke kimuziki. Ni producer mkubwa wa muziki na kazi zake ni pamoja ‘Mapepo, Utamu‘ pamoja na nyinginezo.

“Mimi napenda kazi zote, kuimba na kuwa producer. Lakini wajua mimi nilizaliwa kuimba na napenda sana so nimeanza rasmi kuimba sio kurap tena!:”ameongeza Visita.

Msanii huyo mpya Scar ana album yenye ngoma nne kwa sasa. Je mara yako ya mwisho kuvuta bhangi ni lini? Clemmo akauliza Visita.

“Oooh oohh,aaahhh ammmmhh…ooh siwezi kumbuka hehehe” akacheka Visita kwenye swali alilofikiria kwa zaidi ya dakika mbili.

#MitegoEA

Click: www.fb.com/MkazivaeUNIT