Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Msanii mkongwe kwenye game la muziki Kenya na ambaye ana jina kubwa kwenye ulingo huo ameachia dude jipya.

prezo na clemmo

Prezzo AMB ambaye alishawahi kuhusika kwenye masuala mengi tata ya mahausiano na warembo kibao amempa shavu dada na mtangazaji mahiri wa televisheni,Chess Nthusi.

Mkali huyo wa ‘Za Ovyo’ aliyomshirikisha Bamboo leo studioni pamoja na mtangazaji wa Radio Maisha amefunguaka ya moyoni na kumwaga manyanga kwenye interview moja exclusive kwenye #KonnectTbtParty.

Kwa sasa anamiliki kundi la muziki kwa jina Makini Music Group (MMG) ambapo kwa mujibu wake amesainisha wasanii kadhaa wakiwemo Canibbal na Leon. Ni mwanamuziki rapa ambaye amadumu kwenye game kwa miaka kumi na mitatu sasa bila japo amekana suala ya kufunikwa kimuziki na wasanii wengi wekiwemo undergrounds.

Hata hivyo gwiji huyo mwenye asili ya Kenya na Tanzania, amekiri wazi kuwa yeye sio mtumiaji wa dawa za kulevya kama wanavyodaiwa wala hajawahi kutumia moja ila yeye anajishughulisha na madawa ya mitishamba au ya asili mwendelezo wa kazi ya marehemu babake mmiliki wa Asili Herbal Clinic. CMB yaani Cash Money Brothers ni muungano wao pamoja na wasanii wengine unaokuza muziki nchini.

Dj Young,Prezzo na Clemmo.

Mbali na hayo Prezzo amefunguka kusema kuwa hadi sasa ana ngoma zaidi ya 23 ambazo zipo tayari kwa ajili ya mafans wake.

Leo ametambulisha kazi hio yake mpya ‘Vumilia’ ambayo inatoa faraja kwa mamake mzazi baada ya kufiwa na mumewe ambaye ndiye babake Prezzo.

“Wajua baada ya babangu kufariki ilibidi nimtunze mamangu na kwa ngoma hii nampa uvumilivu na faraja moyoni mwake. Pia ni ujumbe wa kutia moyo watu wanaopitia mambo mazito maishani tuseme mtu kapoteza job, kashindwa kwenye uchaguzi nakadhalika”ameongeza Prezzo.

Msanii huyo pia amekiri kuwa yeye ni Mama’s boy kwani amelelewa na mamake mzazi tangu utotoni baada ya kufariki baba yake.

#MitegoEA.

Click:www.fb,com/MkazivaeUNIT

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.