Mwimbaji wa wimbo ‘Yalio Ndwele Sipite’ amefunguka na kusema kuwa yeye sio mkamba.

Nick, Mc Njaggy na Alex.

Kupitia #Maisha Concert Friday leo ndani ya Radio Maisha, Alex na Nick Odhiambo wememhoji mchekeshaji huyo kutoka Meru ambaye kwa sasa ana trend kwenye mitandao kutokana na wimbo wake huo wenye ujumbe kutokana na matamshi ya mgombea kiti cha ugavana kaunti ya Machakos, Bi.Wavinya Ndeti.

 ‘Yalio Ndwele Sipite’ ni msemo uliotaniwa kutokana na msemo halisi wa ‘Yaliyopita sio ndwele’. Mc Njaggy ambaye ni mcheshi mno alizaliwa mwaka 1988 na ameishi pia Kikuyu na Ukambani.

Je we ni mkamba au vipi? Alex Mwakideu alimhoji. “Mimi sio mkamba lakini nimeishi kwingi kama Kikuyu pia saa hizi niko ukambani. Napenda wakamba sana hata huwa natamani kama naweza geuka mkamba tu” amejibu Mc Njaggy

Ameongezea kusema kuwa ngoma za kikamba huwa tamu zina mvuto na swag kali ya kitofauti ndo maana huwa zina trend kutokana la matamshi na lugha yenyewe kama hio ngoma yake anayotaja rais mpya wa Marekani ‘Tilambu’ yaani Trump.

Mc Njaggy na Nick.

Hata hivyo Njaggy amefungukia suala la mahusiano yake na wazazi wake ambapo amesema mama yake mzazi alimkimbia kutokana na taabu za maisha. Ni msanii mwenye talanta kubwa kwani ndiye aliyeimba remix ya ‘Nerea’ ya Sauti Sol. Pia ni mkali wa freestyle beats yoyote ya bongo fleva anachana nayo tu.

Tazama video yake hapa ya ‘Yalio Ndwele Sipite’.

#MitegoEA.

Click: www.fb.com/MkazivaeUNIT