Kutoka bongo ni story kuhusu msanii mmoja gwiji aliyewahi kufanya vizuri kwenye game la muziki na bado anazidi kutisha kinoma kwenye Sanaa.

Mkali huyo kutokea Marekani ametua Afrika Mashariki nchini Tanzania baada ya aliyekuwa mchezaji wa Manchester United pamoja na klub ya soka ya Real Mdrid, David Beckham kuzuru taifa hilo kimya kimya ili kujivinjari na familia yake.

Tanzania imekuwa kivutio kikubwa cha watalii kutoka mataifa mbalimbali hususan maeneo ya Serengeti National Park na Mlima Kilimanjaro

huyoo.jpg
Usher Raymond

Usher Raymond msanii maarufu duniani naye anafurahia mazingira ya bongo kwani kupitia twitter handle yake ameandika “So amazing to experience this beauty with my family” wakati akiwa katika hifadhi ya taifa ya Serengeti.

yyy

Hata hivyo taarifa za Mr Raymond kuwepo Dar es Saalam zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii na kuwafikia watu wengi kulinganisha na ujio wake mchezaji wa Liverpool Mamadou Sakho lakini pia nyota wa Everton Morgan Schneiderlin na wengineo wengi kama Wayne Roony  ambaye kwa sasa yumo Tanzania kwa ajili ya mechi yao (Everton) dhidi ya mabingwa wa SportPesa super cup, Gor Mahia.