Afrika kuna kila ya madini, muziki, utamaduni na watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya makuu ikiwemo kukujengea furaha yako.

Je una uhafamu mzuri wa muziki wa Kenya na kama hufamu basi nikujuze kuhusu ujio mpya wa mkali wa ‘Bank Otuch’ msanii aliyewahi kuwa hawker mitaani kutafuta shilingi kukidhi mahitaji yake.

bank otuch.jpg

Ochieng Victor Ondeye aka Vicmass Luo Dollah, ni mmojawapo wa wasanii wa Afro hip hop mastaa kwenye ubora wake kutokana na kipaji chake cha Sanaa ya muziki. Afrika Mashariki amekuwa gumzo kwani ameachia track mbili mpya kwa wakati mmoja.

Mwimbaji huyo kwa sasa anachukua headlines kutokana na hatua yake hio ya kuachia nyimbo ‘Call You Mama na Rocking Kitenge(Akala)’ na kuachia video za hizo ngoma kwa mpigo.

Luo Dollah anaamini kwamba msanii ana majukumu kwenye jamii na hivyo anastahili kuwajibika kuelimisha wana jamii kupitia kazi yake ili wengine wapate mfano bora wa kuiga wakiwemo wasanii underground wanaotegemea makubwa kutoka kwake.

“Unajua mimi niliget inspired na msanii Octopizzo the way anafanya kazi yake kwa kujiamini na muziki wenye kuelimisha jamii, so mimi napenda kufanya kazi bora zaidi kuburudisha na kuleta jamii pamoja” amesema Vicmass huku akisisitiza kuwa hio ni style yake mpya ya kuachia ngoma mbili mbili kwani sio kawaida ya kila msanii.

#MitegoEA.

Click:www.facebok.com/MkazivaeUNIT