Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Unafahamu ni jambo la kawaida kwa mwanadamu kukaa bila kuwa mahusiano ya mapenzi kwa muda mrefu?

tande.jpg
Sanaipei Tande

Haya haya hapa yanamhusu msanii wa kike Kenya Sanaipei Tande ambaye anafanya vizuri kwenye game la muziki juzi tu ametokea bongo kuachia kazi mpya.

Amefunguka kusema kuwa yeye kwa sasa hana mpenzi kwa muda wa miaka mitano na hataki kuchaguliwa mwanaume bali yeye ajichagulie umpendaye. Kwa mujibu wake huenda akawa na dume lake mwishoni mwa huu mwaka na kupata mtoto wakati akishapunguza mzigo wa kazi zake anazozikabili kwa sasa.

“Kwa sasa sina mwanaume kwa sababu nina projects kadhaa nafanya lakini December naweza kuwa na mmoja na pia kitumbo hahaha” amesema Sanaipei wakati akiwa kwenye interview Radio Maisha na Alex na Nick.

Tande ni msanii asiye kubali mahusiano ya mapenzi na wenzake wa kazi kwani anaamini kuwa kazini ni sehemu ya kujijenga wala sio mapenzi. Sanaipei aka Natasha amepiga collabo na msanii wa Tanzania, Chege Chigunda ‘Najiuliza’ na sasa upo tayari na video kwenye YouTube.

#MitegoEA

Please leave your comment and share post kindly

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.