Mkali wa ‘Mugacherere’ Qboy Msafi ngoma aliyowapa shavu Shetta pamoja na Rayvanny amezungumzia kuhusu thamani ya meno yake ya chuma.

IMG_6847.JPG
Shugaboy na Qboy Msafi

Qboy ndani ya Radio Maisha amefungukia swali la Clemmo 254 na kusema kuwa yeye yake sio mapambo ila ni grills za meno ya kudumu kwani muda wote anayo.

“Yangu ni meno nilinunua sio mapambo kama wasanii wengine. Mimi nakaa nayo muda wote, usiku, mchana hata napiga mswaki yakiwa mdomoni. Ni grillz zenye gharama ya $200 sawa na Ksh20,000” amefunguka Msafi.

Hata hivyo hajasita kusema kuwa mbali na kazi yake ya muziki na mapambo kwa maana ya stylist na fashion designer anafanya pia kazi ya uongozaji video yaani ni director wa videos na ndiye ameongoza video ya msanii Young Dee ‘Bongo Bahati Mbaya (BBM).

Na MkazivaeUNIT

MitegoEA

Subscribe to our new YouTube channel: MITEGO SASA twendwe sawa