Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Wikendi imekuwa kubwa aisee na mengi ya kusimuliwa yametukia kwenye sehemu mbalimbali za nchi na hapa jijini Nairobi kuliwaka.

Jumamosi ya tarehe 22, July 2017 historia imeandikishwa kupitia bonge la show lililomshirikisha msanii mkubwa kutoka Nigeria.

Wizkid1.jpg
Wizkid

Wizkid aka Star Boy alikiwasha kwenye ukumbi wa KICC wakati alipofika hapo mwendo wa saa  sita mchana hadi kumi na mbili jioni. Mkali huyo aliporomosha burudani kwa takribani saa moja na nusu bila support ya dancers wala backup artists.

star boy.jpg

Wasanii wengine waliokuwepo live stage ni kama Redsan, Willy Paul na wengineo wengi waliomsindikiza walipata nafasi kuonyesha uwezo wako kwenye jukwa hilo.

Hata hivyo jana JumaPili kumeibuka habari za afisa mmoja wa polisi aliyempiga risasi na kuua mwanamke mmoja kwenye gate la jingo hilo la KICC kwa kile ninachodaiwa kuwa ni afisa ambaye alikuwa na ugomvi na dereva wa gari Fulani japo haijawekwa sawa chanzo cha uhasama wao uliosababisha kifo cha mwanamke huyo. Maafisa wa usalama wana chunguza tukio hilo baada ya kuandikishwa statement kwenye Central Police Station.

Wizkid leo asubuhi naye ametoa shukrani zake kwa watu wa Nairobi kwa kuonyesha upendo kuhudhuria show hio yake na kupitia kwa twitter account yake amepost hivi; >”Thank u Nairobi. U guys got the best vibe!!! Kenya love! ?”

#MItegoEA

Subscribe to my YouTube channel, MITEGO SASA>https://www.youtube.com/channel/UCLerJ63TxCYhYQ5UgK3jVGw/featured

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.