Mwimbaji muziki wa kizazi kipya ambaye ni mwanadada mwenye uraia pacha amefungukia suala la kutongoza wanaume.

Kupitia Konnect show Radio Maisha, mwimbaji huyo wa ngoma kama, ‘Duka, Ooh Lala Oui Oui’ amemwaga moyo wake na kusema mengi kuhusu muziki wake na familia yake ambayo ipo Kenya japo kuwa yeye ana uraia wa Ufaransa na Sudan.

Amezungumzia jinsi anavyoitwa mzungu na waafrika kutokana na rangiya  ngozi yake kama yawazungu lakini akifika Uingereza au Marekani, anajikuta anaitwa mwafrika tu.

Yvonne Darcq, amekiri wazi kuwahi kutongoza mwanaume wakati akiulizwa maswali kumi noma ya show hio ya Mwende Macharia na Clemmo 254.

Hata hivyo ametambulisha muziki wake mpya ‘Fearless’ ambayo imechanganya lugha nne tofauti; Kiswahili, English, French na Arabic.

 

MitegoEA

www.facebook.com/MitegoSasa