Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Audition za Kaka Empire zilizofanyika Jumatatu ziliishia kumsainisha msanii huyu ambaye anajituma kinoma kwenye game muziki na sasa ana ngoma mpya.

King Kaka alikuwa ametangaza kuhusu audition hizo ambapo Arrow Bwoy aliibukia mshindi na kusainishwa kwenye lebo hio yake huku bado akiwa kwenye lebo yake ya awali ya Fast Cash Music Group (FCMG).

Kwa mujibu wa Arrow Bwoy ni kwamba alikutana na King Kaka kwenye tamasha la msanii Owago ndani ya SkyLux wakati wa sherehe ya kumbusha la siku ya kuzaliwa kwake. ‘Hapo ndio nilikutana na King Kaka nilipopiga show hapo na baadae akanipigia simu akaniambia amependa kazi yangu hivyo tunaweza fanya kazi pamoja’ akasema Bwoy.

Ni msanii mwenye bidii mno kwani alianza kwa kuuza makopo ‘Scraps’ za vyuma ili kukidhi mahitaji, mara akawa muuza nyama kwa bucha City Park Nairobi ili kuwapata pesa ya kulipia studio.

Kwa sasa ana ngoma mpya baada ya ‘Koona, Bila Bonus’ anatesa na wimbo ‘Murder’ ambao ameutambulisha rasmi ndani ya Konnect, Radio Maisha.

MitegoEA.

 

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.