Janet Otieno

Janet Otieno msanii maarufu kupitia kazi zake nyingi za kumsifu Mungu, ametambulisha ujio wake huo mpya ndani ya Radio Maisha, Maisha Concert Friday kipindi cha Alex Mwakideu na Nick Odhiambo.

Nick, Janet na Mwakideu

Mwimbaji huyo ameachia ‘Shuka’ wimbo ambao unazungumzia jinsi watu wanavyofuata mambo ya duniani na kushahau kuwa kuna Mungu mkuu zaidi ya viongozi au vyama vya kisiasa.

‘Shuka ni ngoma inayozungumzia vile watu wamepotoka kisa masuala ya dunia kama vile siasa na wanasahau kuwa kuna Mungu mkuu kuliko wanasiasa au vyama vya kisaisa, hivyo Mungu anafaa kushuka kuwakomboa wanae’ amesema Otieno.

Hata hivyo amewasihi kudumisha amani kwa kila Mkenya haswa msimu huu wa uchaguzi na kila mwenye kura apige ili kuwe na uchaguzi mzuri na wala watu wasipiganie uchaguzi. >>Subscribe my YouTube channel: https://www.youtube.com/channel/UCLerJ63TxCYhYQ5UgK3jVGw/videos

Boss MOG, Janet na Nexx Le

MitegoEA.