Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Wimbo mpya wa Roma  Mkatoliki?

Roma Mkatoliki.

?Wengi mlijiuliza waloniteka ni Askari

Mkanitafuta vituo vyote central hadi Staki shari

Wakasema hawajui nilipo mama alienda hadi mochwari.

(Daaaaah)

Ya kaisari muachie kaisari ,machozi yenu yatalipwa

Mi nafunga na kusali

(Imba Roma imba x3)

Mungu wa Paulo ndo Mungu wa Daudi

Na ndo Mungu wa John mnayemuita Yohana Wayahudi

Mwanangu alimuuliza mama baba lini atarudi

Na mke wangu aliwaliza kuwashukuru sina budi

Fahamu kuwa mimi siyo rapa tu ni baba wa familia

Na Watoto mahitaji nawapa kama isemavyo Biblia
Je

Kipi bora nife mseme nilikufa kiharakati?

Siogopi kufa ila nawaachaje waliobaki?

Je

Nani kati yenu mwabangu atampa malezi?

Wapi atapata mahitaji? Wapi atapata mapenzi?

Mama naye wapi atapata mahitaji na malezi?

Na ripoti ya upelelezi vipi akiiteka mtekaji?

Je

Kaburi langu mtalipalilia majani?

Nimeumwa hamjakuja niona mnangoja mje msibani ee?

Nilipokuwepo sikuwa najua hii saa nne hii saa nane

Nilichohitaji nitoke mzima na ndugu zangu tuonane

Nimechapwa mijeledi ,nimevunjwa bila huruma

Asante mlopaza sauti nimeiona nguvu ya umma

Siku tatu nimefungwa macho mikoni imefungwa nyuma
Chorus

?Nakwendaaa Zimbabweee Zimbombo

Iyelele mama weee x4

Imba Roma Imbaaaaa

Aaaaaaah Aaaaah

Eeeeehee Roma

(Sema baba wee)
Nasimama na ninaunga hoja kwenye uchumi wa viwanda

Na nanasi linaoza Msoga, tikiti linaoza shamba

Walioniteka hawakuja na Noah ni uvumi na visanga

Ila kutekana tekana huu ni uhuni wa kishamba

Weka bunduki chini si tubishane kwa hoja

Maana sote lengo letu kuijenga Tanzania moja

Mi sikuona nyota kwa shoulder ila najua we ni solder

Inshaallah

Ulikuja mwenyewe au ulipewa order? (ewala)

Aminini siku hazigandi

We ni Yanga mimi Simba kuwa mpinzani siyo dhambi

Ipo siku mtawala atakuwa mpinzani

Simba akichukua kombe sijui atapona nani!

Na kuna mbunge alisema nimemtukana mkuu

Utakuhukumiwa na mkono wa Mungu

Namshitakia aliye juu

Kwanza lini?

Na kwa nini?

Mi nimtukane Mjomba?

Umepewa gari ya wagonjwa mi Tanga wananijengea bomba

Mi mbarikiwa na nikifa kuume kwa Baba nitaketi

Na mtu wa watu that’s why lilisimama Bunge la bajeti

Kunijadili Mtanzania kuwa makini pia

Makinikia nayatungia kuwa mapini pia

Nilitabiri utaitwa Rais kipindi ukiwa Waziri

Japo maisha siyo rahisi ila pongezi unastahili

Na waliosadiki Roma ataonekana kabla ya jumapili

God bless imetimia Injili niliyoitabiri

 

Chorus

?Nakwendaa Zimbabweee  Zimbombo

Iyelele Mama weee x4

Aaaaah Aaaaah

Eeeeehee Roma

(Sema baba wee)

Na; Juma Jr Tz Promoter.

#MitegoEA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.