Fid Q mkali wa ‘Sheri’ wimbo aliyoshirikishwa na Rich Mavoko kutoka Wcb Wasafi ameachia ngoma mpya inayotisha kwenye anga za burudani za zaidi kwenye media mbalimbali.

FID Q

 

Fid Q aka Ngosha ndiye mwanzilishi wa lebo ya muziki kampuni kwa jina la ‘Cheusi Dawa’ ambayo inahusika haswa na kusaidia kukuza vipaji vya muziki mitaani miongoni mwa wanajamii wakiwemo wasanii wachanga.

Ni msanii mkuu wa Hip Hop ambaye amedumu sana kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya hip hop bongo kwani anafahamika kwingi kupitia talanta yake hio ya muziki mzuri.

Ngosha baada ya kuachia video ya ‘Sheri’ amerudi na kali zaidi kwa jina ‘Fresh’ na tayari ina video kwenye YouTube na hadi sasa imewahi views  elfu arobaini na tano kwa siku moja tu.

Hii hapa chini utazame kisha usambaze upendo kwa marafiki zako wote.

#MitegoEA.

@FID Q