Wanaharakati kibao na pia wasanii wengi wamejitokeza na kuzungumzia suala nzima la uchaguzi na matukio ya mauwaji Kenya baada ya rais Uhuru Kenyatta kutangazwa rais kwa awamu ya pili kuwa mujibu ya matokeo ya IEBC.

Wasanii kama King Kaka, Octopizzo, na wengineo wetoa kauli zau za kuwaomba wakenya kudumisha amani lakini pia polisi kusitisha mauwaji ya kupiga raia risasi wanapokuwa wanaandamana.

Jahmbee

Faya Mama aka Jahmbee Koikai kupitia KonnectGetsReal ndani ya Radio Maisha amezungumzia masuala na majukumu ya vijana wakati huu wa taharuki la uchaguzi. Faya Mama ambaye ana shahada zaidi ya tatu amewasihi vijana kuonyesha upendo na kuwa na umoja ili kudumisha amani na kusaidia kuleta utangamano wa wakenya.

Ni zaidi ya activist kwani Faya Mama licha ya kuwa anatokea kwenye vitongozi duni vya Kawangware Nairobi anajivunia maisha yake sehemu hio.

“Napenda Kawangware sana na ndipo nakaa mimi. Nimelelewa hapo na pia wazazi na babu zangu walikuwa anaishi hapo. Not unless niolewe sehemu ya mbali siwezi kuhama Ungwaro” amesema Jahmbee.

Pamoja na vyeti vyake hivyo vya digirii ya French, Communication na International Relationship, pia anapenda sana muziki wa reggae kwani anasema unakuwa na ujumbe mzuri kwenye maisha jamii. Amefungukia suala la kuachia ngoma zake za reggae karibuni.

“Reggae napenda sana coz its true music na inazungumzia what happens in our society and our daily lifes” ameongezea kuwa amekuwa na matatizo ya kiafya baada ya kuugua ugonjwa wa hedhi yake unaosababisha kufanyiwa upasuaji hadi kwenye mdomo.

Hata hivyo amehimiza ushirikiano wa vijana na kutambua majukumu yao katika jamii na sio kubebwa na upepo wa siasa na kudhulumiwa na wanasiasa kwa kuwahonga kuvuruga amani nchi.

“Wajua vijana wanafaa kujua ni nini muhimu kwako, mtu akisema msiende kazini utakula nini na pia utapoteza kazi na wanasiasa hao wana mali zao kwao hiyo vijana wafikirie na wafanye kazi maana watu ubadilika, serikali ubadilika na pia wanasiasa” amemaliza hivyo Faya Mama Jahmbee.

#MitegoEA.