Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Ni kwenye zoezi nzima la upigaji kura mwaka huu 2017 ndipo raia wa Kenya amepata sifa tele na kusambaa kila kona ya mitandao na media kadhaa nchini.

Martin Kamotho

Martin Kamotho amebahatika kuwa miongoni mwa watu wanaozungumziwa mno kwenye mada mbalimbali kutokana na kitendo chake cja kuoenaka kimasomaso akiwa na mfuko wa githeri kwenye foleni ya kupiga kura. Kwa sasa amefanyiwa kila aina ya mzaha lakini pia kuonekana mtu wa tofauti kwani watu walitafsiri tofauti hali yake hio ya kula githeri hadharani. Hali hio imechangia mkurupuko wa mawazo na maoni kizani hadi kuishia kuitwa ‘Githeri Man’ na picha zake kugeuza geuza kwenye photoshop ili watu kuzidi kumfanya maarufu au labda kumfanyia masiahara.

Photoshop za Githeri Man

Githeri Man akikuwa kwenye media mbalimbali kuhojiwa nini kiini cha yeye kuwa na mfuko wa githeri kwenye foleni siku hio ya uchaguzi lakini pia inasemekana imeshaingia dili za kibiashara na makampuni mengi ili kufanya mauzo ya bidhaa zao kutokana na sifa zake kwa sasa. hata hivyo, Kamotho alitunukiwa simu ya aina ya smartphone na kampuni ya huduma za mawasiliano nchini, Safaricom, simu ya bei Galaxy Edge S8.

Githeri Man akielekea kupiga kura

Baada ya sifa zake zote hizo, mtangazaji maarufu kwenye ucheshi wake kwenye radio ya Hot 96, Jalang’o Mwenye amefungua roho na kumwambia Githeri Man kuwa hizo sifa anazo kwa sasa ni kama theluji kwenye simu wa kiangazi,yaani zitayeyuka tu muda si mrefu kwani wakenya ni watu wa ajabu na wanaokwenda na wakati na hivyo hatoweza kuziendeleza kwa kipindi kirefu.

Githeri Man na Jalang’o

#MitegoEA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.

3 COMMENTS

Comments are closed.