Katuni ya Madee na Wolper

Wimbo wenye video ya aina ya katuni yaani animation kutoka kwa msanii ‘rais’ wa Manzese nchini Tanzania aliyomshirikisha staa wa Nigeria, Tekno Miles umezua balaa.

Rais wa Manzese

Baada ya dili yake Diamond Platnumz kufanikiwa, wasanii hao wawili waliingia kazini na kutua mzigo mkali video na audio bora kabisa kwa jina ‘Sikila’. Madee kwa sasa anakabilia na hali ngumu kwa kitendo chake cha kutofuata utaratibu kwenye kutumia picha ya msanii mwigizaji wa bongo movie, Jacqueline Wolper kama katuni bila idhini yake.

Ex-wake Harmonize

Wolper ametangaza kumshatki msanii huyo kwa kumhujumu bila ridhaa yake wala makubaliano yoyote japo kuwa Madee anadai alishamfahamisha kuhusu picha yake kuhusika kwenye video hio yao mpya.

“Niliamua kumtumia Jacqueline Wolper baada ya ‘director’ kuniambia nitafugte picha ya msanii yeyote maarufu ndipo nikaamua kumpatia picha ya ya Wolper na kabla ya kumtumia nilimpigia simu, nikampa taarifa ili aelewe kinachoendelea” asema Madee.

#MitegoEA.