Diamond Platnumz apata wakati mgumu kwani anasukumwa kila pande sio maadui wake tu lakini pia na wasanii wa karibu yake.

Penzi lake na mfanyabiashara wa South Africa raia wa Uganda, Zari The Boss Lady limenoga na kufikia hatua ya kuvujisha matone ya damu za wabaya wao.

Imeibuka ngoma mpya ya wasanii wawili wa hip hop bongo Tanzania huku wakizungumzia wasanii na watu maarufu nchini humo na kuonekana kama ndo kwanza wanasaka kiki.

Roma Mkatoliki amempa shavu mwenzake Stamina kwenye collabo yao kwa jina ‘Huku Ama Kule‘. “Hizi ama Zile, Huku ama Kule, shavu nyingi ziko  wapi Roma Huku ama Kule, Zinanichanganya sijui ni huku ama kule maana nazoskia huku  ndo nazoskia kule….” wanachana wasanii hao.

Stamina na Roma

Kitu cha ajabu ni kuwa wasanii hao wametokea studioni moja ya radio huku wamevalia masweta yenye majina ya wapenzi wa Diamond aka Simba. Stamina kavalia sweta yenye jina la Zari mgongoni naye Roma yenye jina la Wema ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond kipindi cha nyuma kabla ya Zari.

Histoshe kwenye michano yao wamewataja wastaa wengine kama vile Ronaldo, Messi, Giggy Money, Snura na pia rais Magufuli na Lowassa.

Je wanasaka bifu kwa Simba au ndio kutafuta kiki kwa majina ya wenyewe?

1 COMMENT

Comments are closed.