Afrika Mashariki kunazidi kuzaliwa vipaji vingi na kukuza mastaa kwenye tasnia ya muziki na burudani kwani waimbaji wengi wanazidi kuonyesha uwezo wao.

Mwanadada Mkenya nyota wa muziki na filamu sasa amevuka boda hadi Uganda na kuachia collabo moto ambayo imeanza kuwa gumzo kwenye mitandao namedia tofauti.

A Pass na Avril

Avril, baada ya kutoka na ‘Uko’ na kuteka anga za burudani Afrika Mashariki, amezidisha mwendo na hatua yake nyingine ni collabo yake na staa wa dancehall Uganda, A Pass.

Wawili hao wameachia hit song ‘Babiee’ ngoma ya kucheza kwa klub lakini pia kutesa kwenye radio stations kwani mwingiliano wao kimuziki uko vizuri sana.

Audio ni kazi ya mikono yake mtayarishaji Saint P huku video hio kali mno ikiandaliwa na kuongozwa na J Blessings katika ukumbi wa Magic Planet Game Arcade, Two Rivers Nairobi. Ni wimbo wa kiswahili na kiingereza.

Kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii, wakali hao wamefunguka kuhus collabo hio yao.

” Working with Apass was amazing. his work ethic and great spirit just made everything work so well. I am humbled to have worked on a song with him,” asema Avril. naye A Pass akimwaga ya moyoni kuhusu Avril.

” I was so humbled to work with Avril and her whole team. It was amazing. It is amazing how music works, you don’t know someone they don’t know you but they know your music and like what you do and you happen to like what they do as well. It was a very good project to do, I give thanks.” akamaliza hivyo A Pass.

#MitegoEA.

1 COMMENT

Comments are closed.