Malimwengu hayatawahi kuisha kutokana na vitendo vya wanadamu wengine wenye hulka ya utani na ucheshi mwingi.

Ni rahisi kuona mtu akibeba wasaifu wake kuelekea kuomba au kusaka nafasi za kazi katika idara na afisi mbalimbali ilmradi akithi mahutaji yake na kufikia malengo ya maisha yake.

Jamaa akikabidhi CV kwa majiri.

Watu wameshaingiwa na tabia ya kulaghai huku wengine wakiishia kuhonga waajiri ili kuwahi nafasi kwenye makampuni makubwa bila waajiri hao kuzingatia uzoefu, tajriba na uelewa, sifa za mwomba kazi husika.

Huyu jamaa hapa kwenye video anaonekana kuchanganyikiwa na kushindwa kumudu pipu ya maji kutokana na presha ya maji kubwa na kumbwaga chini na kumloesha maji huku msimamizi wake akimcheka na kumdhihaki kwani alifumbua kumbua kuwa hana ujuzi wowote wa kufanya kazi na mabomba ya maji au kusafisha magari na sakafu kwa kutumia njia za kiteknolojia.

#MitegoEA.