Diamond Platnumz amekuwa jina tajika na kila mtu haswa mabinti wanajipa vijisababu vya kulitumia jina lake kujitafutia kiki au sifa.

 

Kisa cha mtoto mchanga kupewe jina la staa huyo muziki duniani kutokea bongo Tanzania Nassib Abdul bado kimebaki kitendawili huku wawili hao, Diamond na mama mtoto Hamisa Mobetto ambaye pia ni mwanamitindo na video queen kwenye video ya wimbo ‘Salome’ wakizidi kuacha wengi vinywa wazi.

Hamisa amekuwa akichukua headlines kutokana na kujifungua mtoto huyo na kudai ni mwanae Simba Diamond Platnumz na ambaye inafahamika wazi ana familia na mwanabiashara, Zari The Boss Lady ambapo pia wamebarikiwa na watoto wawili; Tiffah na Nillan.

Diamond, Hamisa na Zari

Hatua za kubainisha haswa ukweli kama Hamisa amejifungua mtoto damu ya Diamond imekuwa shughuli pevu kwani Diamond ananekana kukubali kwamba ni wake lakini hapo awali alimtukana na kusema kuwa  ‘A Bitch is Dying for fame’ pia Hamisa anakaa kukana sio wa Diamond.

Katika harakati za kutafuta ukweli, mama yake mzazi Diamond Platnumz amelizungumzia suala hilo huku akionyesha furaha ya kupata mjukuu wa kiume kwa maana ya ‘Mume’ lakini pia mzee Abdul Juma baba yake Platnumz akifunguka na kusema kuwa mtoto wake Diamond sio dhambi akiwa na watoto kutoka kwa wanawake tofauti kwani dini yao ya kiislam inaruhusu.

“Diamond ni mtoto wa kiume na pia ni mwislam na dini inaruhusu hata awe na wanawake sita kwani anajiweza ana mali nyingi, cha msingi tu awatunze na kuwapa riziki yao. Nassib anajua kinachoendela ndo maana hajakurupukia kusema chochote” ameongeza kusema kuwa mtoto huyo kupewa jina la ukoo wao haswa Abdul ambalo ni jina lake inaaleta hishima kubwa kwake kwani inonyesha bado Diamond anampenda.

Harmonize na Diamond

Hata hivyo kwenye kunyapia nyapia mitandaoni nimekutana na maandishi baina ya Diamond Platnumz na msanii chini ya lebo ya Wcb Wasafi, Harmonize akitisha kumtimua kwenye lebo hio yake kutokana na ujumbe wake kwenye whatsApp akimhoji kuhusu mimba na mtoto huyo anayesingisiwa ni wake. Tazama;

#MitegoEA.

1 COMMENT

Comments are closed.