Its another one kutoka bongo muziki mzuri wa bongo fleva ambapo video mpya msanii alifanya remix ya ‘Karorero‘ pamoja na msanii wa Kenya, Naiboi, ameachia mpya.

Qboy Msafi

Qboy Msafi aliyekuwa chini ya lebo kali ya Wcb Wasafi na baadae kutimuliwa kwa madai ya kutaka kuimba wakati anaambiwa na wenzake hana kipaji cha kuimba bali cha kuwa msanii wa mitindo yaani stylist kwenye kampuni hio, sasa amezidisha ukali wake na kudhihirisha kipaji anacho kutoka kwa maulana.

“Unaanzaje kumkufuru mungu, utakosaje kumshukuru…” ndio sehemu ya wimbo wake huo mpya kwa jina ‘Unaanzaje’.

Qboy kwa sasa anafanya kuziki kama msanii wa kujitegemea na kweli anafanya kila awezalo kuhakikisha wewe shabiki na mdau wa muziki unafikiwa na kazi safi yenye ladha tele kwa kuwa amejipanga ili kukupa burudani.

Director wa video ni Mims huku audio chini ya Mr T Touch. Itazeme hapa chini.

#MitegoEA.