Simba aka Diamond amekuwa trending kila sehemu baada ya skendo kali kuhusu mtoto wa Hamisa Mobetto ambapo hajaweka wazi wala kupinga kuwa sio mtoto wake kwani hata ana jina la baba yake mzazi, Abdul.

Diamond

“Baba Tiffah mtaniita baba Nillan, naskia naitwa baba Abdul, kuna mambo mtaani,, haha” akarap kwenye verse yake Diamond.

Hata hivyo kuna wimbo mpya una vuma remix ya Freshi ngoma yake staa wa hip hop Tz, Fareed Kubanda aka Fid Q ambapo Diamond ndiye aliyemuomba wafanye remix hio.

Fid Q

Suala nzito ni pale Simba anapo diss msanii staa mwenzake, Ali Kiba kwa kusema asifanannishwe na ‘Cinderella’ akimaanisha Ali Kiba kutokana na ngoma iliyompa sifa na kumtambulisha kwenye muziki.

“Naona swala wanafosi tuwe sale sale, viuono vidogo wanataka penzi la pepe kalee, si walitaka kiti, nimewapa hadi kitanda wakalale”.amerap Platnumz

Hii ninaleta picha ya bifu kali lake Diamond na Ali Kiba ambalo tena Diamond amelichochea moto tena. Ali Kiba kuna kipindi alikuwa kimya kimuziki kwa muda mrefu baadae akarudi na ngoma ‘Mwana’ na hapo akawa anapata interviews nyingi mpaka kwa The Sporah Show aliposema kuwa kiti chake kimekaliwa na amerudi rasmi kukichukua.

Ali Kiba

 

Lakini pia inaonekana Platnumz amewalenga wasanii wawili ambao hawako poa kimuziki wao kutokana na bifu nzito na mwingine amelengwa ni Ommy Dimpoz mkali wa ngoma ‘Cheche’.

Ommy Dimpoz

Inasemekana mistari ya rap kwenye Fresh Remix, Diamond ameandikiwa na Rayvanny ambaye pia amekaa kwenye chorus ya wimbo huo ambao bado video yake kuachiwa.

Rayvanny

#MitegoEA.

1 COMMENT

Comments are closed.