Augustine Kelechi Miles mkali wa ‘Pana,Duro,Diana‘ ambaye ni bonge la msanii mwenye jina tajika kutoka nchini Nigeria atakuwa akikupakulia collabo moto na msanii wa Wcb Wasafi.

Tekno

Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa anatesa anga na kibao chake kwa jina ‘Sina’ ambacho kinamhusisha msanii wa kutoka enzi, Mr Nice kwenye taswira ya mtu aliyekuwa tajiri mkubwa kutokana na mafanikio kwenye muziki, hatimaye akapandwa na kiburi na kutumia mali yake vibaya hadi akaishiwa.

Harmonize na Krizbeatz

Harmonize ameonekana kwenye picha akiwa kwenye studio ya kurekodia muziki ya Tekno Miles Nigeria akiwa na producer wa mkali huyo, Krizbeatz.

Harmonize na Tekno

Wawili hao wanatarajia kuachia collabo pamoja kwani inaonyesha boss waHarmonize, Diamond Platnumz amekwisha kumpa connect kwa mkali huyo wa Nigeria, Tekno.

Sallam na Harmonize Studioni

Hata hivyo manager Sallam ambaye ni manager wa wasanii Wcb Wasafi ameonekana kwenye picha hio kwani aliandamana na Harmonize ili kuhakisha kazi nzuri inafanyika.

Hatimaye mrembo wake Harmonize kutoka Italia, Saraha ana ujauzito na huenda akajifungua mtoto hivi karibuni na Harmonize kuwa mzazi.

Harmonize na Sarah

#MitegoEA.