Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Kumbe sio tu Prezzo mkali wa rap ambaye alimtamani na kumzimia mwanadada Sheila Mwanyigha ambaye ni mtamgazaji wa radio na Tv nchini Kenya.

Mwanamke huyo kwa sasa anajita tajika kwenye media industry ya Kenya lakini pia ni msanii ambaye alikuwa akitoka kimapenzi na msanii Prezzo AMB kabla ya kutengana kisa udanganyifu na ukosefu wa uaminifu kwenye penzi lao.

Prezzo na Sheila

Prezzo ambaye anajigamba kutoka kimapenzi na takriban kila celeb nchini Kenya, ameskika akisema kuwa huenda akarudisha penzi lake kwa Mwanyigha licha ya kuwa majuzi alionekana kwenye msanii wa kuchora Tattoo mwilini, akifuta baadhi ya michora na majina ya wapenzi wanawake wake.

Hata hivyo mkali mwingine wa hip hop Kenya, Khaligraph Jones baada ya tuhuma za kuchubua ngozi yake ametoka wazi na kuelezea hali halisi.

“Mimi sijawahi kubleach skin yangu hata kidogo nashangaa kila mtu anasema Khaligraph amebleach. Nilikuwa interview The Trend, NTV nikapiga picha lakini lighting ya hapo ndani ndio ilireflect sana nikaa kama mzungu” akasema Papa Jones.


 

Pia msanii huyo aliachia wimbo wake kwa jina ‘Khalighraph Amebleach’ ambao ulionyesha kuwa amechubua ngozi yake. Kwa sasa ana video mpya ya ‘Nataka Iyo Doh’.

Khaligraph

Khaligraph amefunguka na kusema kabla hajawa staa alikuwa akimtamani sana Sheila Mwanyigha awe mpenzi wake kipindi cha nyuma kidogo.

Sheila

#MitegoEA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.