Mashabiki wa muziki muziri wa bongo fleva leo Ijumaa watakuwa wanakata kiu cha muda mrefu tangu msanii gwiji wa bongo fleva aachie wimbo wake ‘Aje’.

Kiba

Ali Kiba aka King Kiba ametoa ahadi ya kuwapa kitu kipya mashabiki wake na wadau wa muziki na ujio mpya baada ya kutokea mgogoro kwenye mitandao ya kijamii na pia kwenye media kuhusu bifu lake na Diamond Platnumz kwani alimdiss kwenye ‘Fresh Remix’ ya Fid Q kwamba “walitaka kitu, nimewapa mpaka kitanda wakalale”alirap Diamond.

Baada ya kimya chake Ali, ametangaza ahadi hio jana kupitia vyombo vya habari kuwa mashabiki wake mkao wa kula kupokea hio kazi mpya kwa jina ‘Seduce Me’.

“#SeduceMe Exclusive Premiere Tomorrow 25.08.2017 on AlikibaVEVO & Global Music Stores
Subscribe now on AlikibaVEVO.#RockstarTV #SHOOOOSH #SonyMusicAfrica #RockStar4000 #KingKiba,” aliandika Alikiba kwenye ukrasa wake wa Facebook.

#MitegoEA.