Recording Label ya Rockstar 4000 ambayo yumo msanii wa bongo fleva Ali Kiba imeachia wimbo wa msanii huyo mpya ambao ulitegemewa kuitwa ‘Kipusa’ lakini unakwenda kwa jina la ‘Seduce Me’.

Ali Kiba amekuwa kwenye bifu la muziki na Diamond Platnumz aka ‘Lips Denda’ kwa kipindi kirefu lakini bifu lao linaonekana ni la mzaha tu kwani maneno aliyoyatumia Ali Kiba kwenye ngoma yake hio mpya yalishasemwa kipindi hajaachia wimbo huo na Platnumz kwenye diss track ya ‘Fresh Remix’ ngoma ya hip hop aliyorap Diamond.

“They call me heartbreaker na majina mapya eeeh kila mmoja amenipa..Wananiita kipusa pasua kichwa…” ameimba Ali Kiba.


Ni maneno aliyosemwa na Diamond kumhusu Kiba kabla kuachia wimbo huo mpya. Tazama hapa chini video yake;

#MitegoEA.

1 COMMENT

Comments are closed.