Blessed Njugush aliyesomea uanahabari katika taasisi ya mawasiliano KIMC hatimaye akaishia kuwa comdia na mwigizaji wa filamu Kenya amefunguka mengi live studioni.

Njugush

Akizungumza kwenye Maisha Concert Friday Radio Maisha, Njugush amesema kwa bada ya kuhusika kwenye kipindi cha Hapa Kule News, alifanikiwa kuigiza kwenye kipindi cha televisheni cha Real House Help of kawangware kama muuza malimali.

“Nipokuwa chuoni KIMC, Abel Mutua aliniona na kuniambia sura yangu haipendezi kuwa mwanahabari. Baadae akanipigia simu niwe kwenye kipindi cha House Help Of Kawangware” ameweka wazi Njugush.

Hata hivyo comedian huyo hakuona msaada wa kipindi hicho na hapo ndipo walipoungana vijana watano na kuanzisha comedy zao na kurekod filamu huku wakiomba msaada wa hela ya mtaji ambayo hawakufaulu.

“Nilijitoa mimi na vijana wengine watano tukaanza kushoot movie zetu coz tulikuwa na ideas kali na pia tunajua kuproduce vitu kali lakini tatizo hatukupata capital ya 5m wakati tulianza kuomba msaada watu walituhepa na hatukusaidika” akaongeza Njugush.

Baada ya wasanii hao kutofaulu kupata mtaji huo wa shilingi Milioni tano, waliamua kutumia simu zao kushoot movie hizo na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii ili kuwafikia mashabiki na wapenzi wa comedy na movies kwa wingi. Pia amewasihi vijana kutumia vifaa walivyonavyo vizuri kwa manufaa yao wenyewe sio kuomba vitu nyeti saa sita usiku kwa kutumia bundles.

“Vijana watumie bundles za simu zao kwa vitu positive na creative ili kujiendeleza na sio kuomba ‘vitu nyeti’. Saa sita usiku mtu anakuomba umtumie elfu mbili utatoa wapi kama sio vitu nyeti?” akamaliza hivyo blessed Njugush.

#MitegoEA.