Msanii mmoja wa kike amefunguka ya moyoni na kusema wazi kuwa anaweza kulala kitanda kimoja na gwiji wa muziki wa bongo fleva anayetamba na ‘Seduce Me’.

Mkali huyo amekuwa vinywani mwa watu wengi kuhusu bifu lake na Diamond Platnumz kutokea Wcb Wasafi lakini kwa sasa anatamba na video yake hio mpya kwenye kila mitandao kwa muda mfu tangu kuiachia imewahi zaidi ya views milioni mbili.

Clemmo, Viola na Mwende

Viola Karuri msanii wa Kenya ambaye ndiye kaifanyia haki wimbo ‘Despacito Swahili cover’, kwa swahili version, akiwa Live radio Maisha kupitia Konnect Spicy Monday, amefunguka na kusema hayo kwenye maswali kumi noma.

Karuri ameweka bayana kuwa ikitokea kuwa kwa nyumba yake kunaye msanii Diamond Platnumz aka Lips denda na Ali Kiba  aka King Kiba, anaweza kumchagua Kiba kulala naye kitandani.

Hata hivyo msanii huyo amelizungumzia suala la wasanii kufanya cover za nyimbo za wasanii alipoulizwa kuhusu wimbo mpya kutoka kwa WCB Wasafi ‘Zilipendwa’ na ambao unaleta mgogoro kwani msanii Matonya anasema kuwa huo ni wimbo wake wa zamani na hakushauriwa kabla waendelee kuutumia wasanii wa Wcb.

Viola na DJ Young

“Cover ya wimbo kila mtu anafanya cover lakini hio ya Wcb labda kwa sababu ni next door, wangeshauriana na ikibidi alipane royalties” akasema Karuri.

‘Despacito Swahili’ ni ngoma ya kiingereza ambayo imefanyiwa cover na wasanii tofauti kwa lugha tofauti na hii hapa chini ndio Swahili cover kutoka kwa Viola Karuri.

#MitegoEA.