Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.

Msanii ambaye ameweza kupata fursa ya kuijunga na bunge la Kenya ameachia kazi mpya ambayo aliwaahidi mashabiki wake siku moja tu wakati akila kiapo cha utendakazi tarehe 31/8/2017.

Charles Njagua Kanyi aka Jaguar ametawazwa kuwa mbunge wa eneo bunge la Starehe jijini Nairobi baada ya kumbwaga mpinzani wake Maina Kamanda kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi mwezi Agosti tarehe 8, 2017. Mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa kizazi kipya ameonekana kuendelea na kazi yake ya sanaa licha ya kuapishwa kuwatumikia wananchi na wakazi wa Starehe.

Hon.Jaguar

Hon.Jaguar amefuata nyayo za wasanii wabunge wenzake kama vile Profesa Jay ambaye ni msanii lakini pia mbunge a Mikumi nchini Tanzania. Hon. Bobi Wine amabye pia ni msanii na mbunge nchini Uganda.

Jaguar ameachia wimbo wake mpya kwa jina ‘Ndoto’ akimaanisha kutimia kwa maono yake ya siku za nyuma kwani amefikia alipokuwa akitamani kufikia na sasa ni mheshimiwa.

“Maisha imegeuka sasa nalindwa kama benki, napata heshima toka ghetto mpaka ikulu, sina bifu nao wanaojiita king na mifuko imetoboka, Jaguar ndiye komanda uliza Kamanda.” ameimba Jaguar kwenye wimbo wake huo kutoka Main Switch Production.

Skiliza ngoma hapa chini;

#MitegoEA.

Did you find apk for android? You can find new Free Android Games and apps.