Otile Brown mkali wa muziki nchini Kenya ametenga muda wake na kupiga story na Radio Maisha Asubuhi na kuweka bayana mambo mengi ya muziki na kama hufahamu basi amesema kuwa industry ya muziki Kenya ndio the hardest duniani.

Otile

Msanii huyo anayetamba kwa wimbo ‘Acha Waseme’ ngoma kwa mujibu wake ni ya kawaida na aliiachia kipindi cha uchaguzi Kenya ili wape burudani wananchi na wasahabiki wake baada ya ghasia zilizotokea sehemu tofauti kufuatia matokeo ya uchaguzi na haukua wimbo rasmi kwani atakua anaachia ngoma kali wiki mbili zijazo.

“Wimbo wangu huo mpya sio wimbo mkubwa bali muzki tu wa kawaida ambao nimeona niachie time hii time ya elections ili mafans wapate kitu cha kuwapa raha wakati huu watu wapo na mishe mishe nyingi za uchaguzi” akasema Otile.

Otile pia ameta kuwa tasnia ya muziki Kenya ndio ngumu zaidi duniani na kama ukiona msanii akifanikiwa kimuziki basi mpe na heshima yake kwa sio kitu cha kawaida kwa sababu wapo wasanii wakubwa wafanafanya kazi kwa bidii lakini bado wajapata nafasi ya kupenya kwenye soko la muziki.

“Haijalishi unaimba nini bora kutusua kwenye game la muziki Kenya, coz ni ngumu sana kuona msanii ametoboa. Wapo wasanii wanaimba sana lakini bado hawajapenya kwa kuwa industry ya Kenya ndio hardest duniani. Msanii anakuambia ameachia ngoma yake mpya na inabaikia tu hapo kwa kusema una ngoma ahakuna wa kukupa support” akaongeza Otile.

Hata hivyo amezungumzia penyenye za kuwa amepata ‘Sponsor’ mwanamkwe wa kumlea huku akisema kuwa wanaosema hivyo watoe ushaidi tosha kwani yeye hana maisha hayo ya kulelewa na mijimama ya mitaani ili afaidi mali yao.

“Mimi naskiaga tu watu wanasema nina sponsor jimama mitaani lakini sio kweli coz hakuna evidence. Kiukweli mimi nipo busy kazini najituma kufanya kazi kali kali kama kawaida ya Otile” akamaliza hivyo.

Otile atakuwa anaachia collabo mpya na msanii wa nje ya Kenya ambaye hajamtaja kwani ataka iwe surprise kwa mashabiki wake.

>MitegoEA.