Vituko nchini Kenya ni sehemu ya maisha ya wananchi na vinachangia utengamano na utendakazi kwa uchangamfu kwani vijana wengi hujituma pia kuwa wachekeshaji na kupata kipato cha kujikimu maishani.

Bunge la awamu ya kumi na mbili lilipokuwa linajitayarisha kuanza rasmi kazi, wabunge, magavana, wawakilishi wa wodi, wawakilishi wa wanawake na pia nafasi za waheshimiwa wengineo walipata kula kiapo cha kazi ili kuwawajibikia wananchi kama walivyowaahidi kwenye sera zao wakati wa kampeni.

Tarehe 31, Agosti 2017 mbunge mteule Embakasi, Babu Owino alizua kicheko bungeni akila kiapo wakati alipoapa kwa jina la kiongozi wa upinzani, Raila Odinga badala ya rais Uhuru Kenyatta japo kuwa kuna mvutano wa matokeo ya uchaguzi ya urais baina ya mrengo wa NASA na Jubilee hivyo nafasi ya urais bado kizungumkuti hadi matokeo ya duru ya pili mwezi ujao wa Oktoba.

Babu Owino aliishia kumaliza kuapa kwa msemo wake wa siku zote ambao unatokana na mrengo wa NASA, ‘Tibim’ alipoutamka mbele ya bunge hilo na kuwafanya watu wacheke huku akilazimishwa kurejelea kiapo kwa mara ya pili.

Tazama video hii hapa chini alichokisema;

>MitegoEA