Nachukua nafasi hii nikusute ewe mfanyabiashara ambaye ungependa kuona mafanikio ya kazi ya mikono yako kwani kuna baadhi ya vitu muhumi vya kuzingatia.

Watu walishabadilika na kuanza kuishi maisha ya kinyama kutokana na ugumu wa maisha kwani kila kitu kimegeukia mfumo wa digitali hivyo kuwatenga wasio na uelewa au ufahamu wa kidigitali. Nikiwa jijini nilibahatika kumwona muuza bidhaa kwa street akihudumia mteja wake aliyefika kununua kofia na vitu vingine vya mapambo lakini mwisho wa siku hali ilitibuka na kuanza ugomvi.

Jamaa alifika pale akakagua mali hio iliyokuwa imetandazwa vizuri ili kuvutia wateja wa barabarani ndipo kijana huyo alianza kubahatisha kofia gani inaweza kwendana na mwonekano wake kwa kuzipima hizo kofia kichwani mwake. Mara hii mara ile kwa umakini mkubwa huku muuzaji akijaribu kumshawishi anunue angalau moja.

Jamaa akamwonyesha kijana hadi pete za vidole, saa na pia mikufu ya shingoni ili asiondoke bila kununua japo saa ya mkononi. Hatimaye kijana alishindwa kununua bidhaa zake kutokana na bei ghali ya muuzaji kwani hwakuafikiana bei. Ikabidi kijana aondoke baada ya kukaa hapo kwa muda mrefu akikagua bidhaa na kujaribu kumwelezea kipato chake na angalau waafikiane bei.

Muuzaji alipoona kijana anaondoka bila kununua lolote wala chochote japo ni haki yake kama mnunuaji kujielezea na kutafuta sehemu ya bei anayoweza kumudu, muuzaji alianza kumfokea na kumzomea kwa matusi makali mbele ya wapita njia kisa hakununua kitu hapo hali nilioiona ya kipuuzi sana kwani sio maadaili ya kijamii na mbinu za uuzaji. Muuzaji ana haki ya kumshawishi tu mnunuaji sio kumkashifu na kumzomea mnunuzi kwani atakua amekosa baraka za huyo munuzi hata kama hajanunua. Lugha ya heshima kwenye biashara ni kigezo cha msingi ndipo mwisho wa siku unao watu wakihesabu faida na wengine hasara kutokana na roho zao, lugha chafu na maadili kwenye biashara zao.

>MitegoEA.