Mkali kutoka Nigeria anatua nchini Kenya kwa ajili ya kupiga show la nguvu na kukutana na mashabiki wake wikendi hii.

Wasanii wengi wa Nigeria wakuwa Kenya kutoa burudani ya muziki wao kwa mashabiki kama vile,Iyanya, Wizkid, Davido na sasa zamu ni yake mkali wa ‘Pana’ kuonyesha ubora wake kwenye steji.

Tekno Miles aka Augustine Miles Kelechi atakuwa Live Ngong Rececourse,Water Front Nairobi tarehe 9 huku akiandamana na bendi yake ili kukusogezea bonge la burudani kupitia ngoma zake ambazo zimekuwa maarufu sehemu nyingi za dunia.

Tamasha hilo litaanza saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi alfajiri Jumapili. Wasanii wengine wanaotarajiwa kutumbuiza ni pamoja na;

 • Kansol
 • Creme Dela Creme
 • Kace
 • Xclusive
 • T-Boy
 • Ally Fresh

Watu mashuhuri (VIP) watapata huduma zifuatazo kwa hisani ya Roya Ent na Hype na hakuna tiketi ya VIP itakayo uzwa kwa gate.

 • Lounge and cocktail table seating
 • Own bar
 • Own lavatory
 • Designated parking
 • Close stage proximity
 • Fast tracked access

>MitegoEA.